NEW: Dividend Notice
NICOLNICOLNICOL
Mon - Fri: 9:00 AM - 04.00 PM
invest@nicol.co.tz
Mirambo House 3rd Floor

Questions and answers

Questions and answers

Questions and answers asked at the sixth shareholders' meeting

HALIMA DIWANI MSANGIQuestion: Why electronic meeting?
Read More
Answer: Due to COVID-19 disease outbreak and the whole world suffering from pandemic, we are taking measures to ensure safety of our shareholders by reducing social gatherings and maintaining social distancing.
DISMAS CYRIL MACHAQuestion: my concern is based on the share dividend, I didn’t get the first dividend like other members. I don’t know what happened for me not involved from beginning. I paid my dividend for the second time soon after submitting my bank account. What was the problem?
Read More
Answer: Initially dividend was paid directly through post office. Due to challenges arising from paying dividend through postal address we have opted to pay dividend through bank.
HUSSEIN JUMA KADARIQuestion: Why no dividend till now?
Read More
Answer: Your dividends has paid through your NMB account. Dividend for the year 2016 paid on 8 march 2019 amount 71,250.year 2017 paid on 11 march 2019 amount 74,100.Year 2018 paid on 28 December 2019.year 2020 paid on14 December 2020 amount 28,500.
IBRAHIM ALLY NGOWOQuestion: Why English only. What about those who don't know English?
Read More
Answer: NICOL has both local and foreign shareholders. We use Swahili and English when communicating with our shareholders.
JOHN KIBOKO MUSHIQuestion: Tarehe 15/09/2020 niliomba kubadilisha jina kupitia Core SecuritiesLimited na mpaka sasa wanadai certificate mpya haijatolewa. Je, itachukua muda gani kupatikana? John Alphonce (Kiboko) Mushi
Read More
Answer: Taratibu za kubadilisha jina kwenye cheti cha mwanahisa zinafanywa na Soko la hisa Dar es Salaam (DSE) kupitia madalali wa soko (Stock market brokers). Tunaomba uwasiliane na CORE Securities ili uweze kupata cheti chako.
: AUGUST BENEDICT KOWEROQuestion: I see most other shares entities have paid dividends...
Read More
Answer: Board of Directors recommend the dividend to be paid out to shareholders. Subject to obtaining approval from Annual General Meeting of shareholders, dividend is paid out after the AGM. In most cases, NICOL pays dividend during the last quarter of the year.
HUSSEIN JUMA KADARISwali: Kwa nini Mimi Hussein Juma Kadari mwenye Hisa 1,500 sijawahi kupata GAWIO wala taarifa yenye kueleweka?
Read More
Jibu: Kwa sasa hisa zako ni 3000.Tumetoa gawio kwa miaka minne 2016 gawio ni shilingi 25 kwa hisa,2017 gawio ni shilingi 26 kwa hisa,2018 gawio ni shilingi 6 kwa hisa na 2020 gawio ni shilingi 10 kwa hisa. Magawio yote manne umelipwa kupitia akaunti yako ya NMB. Gawio la 2016 umelipwa 71,250 tarehe 8/3/2019, gawio la 2017 umelipwa74,100 tarehe11/3/2019, gawio la 2018 umelipwa shilingi 17,100 tarehe 28/12/2019 na gawio la 2020 umelipwa shilingi 28,500 tarehe 14/12/2020.
JOHN KARWANI MBYAZITAQuestion:(a):JE NI KWA NINI SHARE ZANGU HAZIONGEZEKI TANGU 03/06/2009?? "NINAOMBA NIJULISHWE SHARE ZANGU MPAKA SASA NI NGAPI?
Read More
Answer: Idadi ya hisa huwa haiongezeki, bali thamani ya hisa ndio inaongezeka bei ya hisa ikipanda. Idadi ya hisa inaongozeka mwanahisa anaponunua hisa nyingine.
JOHN KARWANI MBYAZITAQuestion :(B) (B)NINAOMBA SHARE ZANGU ZOTE NIZIHAMISHIE CRDB BANK PUBLIC LIMITED COMPANY KWENYE CDS ACC.NO 165760.
Read More
Answer:Utaratibu wa kuhamisha hisa unasimamiwa na mawakala wa soko la hisa.Tafadhali wasiliana na wakala mmoja wapo wasoko lahisa ili kupata utaratibu.
JOHN KIBOKO MUSHIQuestion: HIVI KARIBUNI TUMELIPWA GAWIO LA 2016, 2017 NA 2018. JE, MIAKA YA NYUMA KAMA 10 HAPAKUWEPO KITU CHOCHOTE?
Read More
Answer:1.Uwepo wa gawio unatokana na faida itakayoweza kutoa gawio.kampuni ilipitia changamoto za kesi zilizotokana na uongozi uliokuwa madarakani kugoma kutoka madarakani baada ya wanahisa kuutaka uongozi huo kuachia madaraka.Gharama za kesi zilipelekea gharama za kampuni kupanda.
JULIUS LUTA MUSHUMBAQuestion: Kama Corona imeisha kwa nini tufanye kikao on line, au ndiyo kubana matumizi bila idhini ya Wanahisa????????.
Read More
Answer:Corona haijaisha na kama tunavyopata miongozo toka kwa wataalam wa afya kuwa tujikinge kwa kuchukua tahadhari.Kama kampuni tumechukua tahadhari kwa kufanya mkutano kwa njia hiyo.
CHIPOLE DAM CHIURUQuestion 1: Samahani mimi Dam Chiuru naomba kujua kuhusu gawio la 2017 na 2019 sijapata inakuwaje? Asante.
Read More
Answer:1.Gawio la mwaka 2017 umelipwa shilingi 49,400 tarehe 9/4/2019 kupitia akaunti yako ya CRDB.Mwaka 2019 hakukuwa na gawio.
CHIPOLE DAM CHIURUQuestion2:Halafu kuhusu share zangu ziko ngapi? Na tunaomba tupate certificate za share mimi nimepata mpaka sasa moja tu toka nijiunge inakuwaje?
Read More
Answer2:Hisa zako ni 2000,kuhusu cheti tunawasiliana na wewe kwa maelekezo zaidi.
JOSEPH ROBERT SHIJAQuestion: Mi kama mwanahisa naweza kupata mkopo?
Read More
Answer: Ndio, Faida mojawapo ya kumiliki hisa za kampuni iliyoorodheshwa kwenye soko la hisa kama NICOL ni kuzitumia kama dhamana unapotaka kuchukua mkopo kwenye taasisi ya fedha.
REGINA MACHUAQuestion: Awali ya yote niwashukuru uongozi mpya kwa hatua hii mlioifikia ya kuikomboa nicol kwenye mikono ya wajanja wachache. Hongereni sana! Swali langu je ninwezaje kupata statement yangu? Na kuna mpango wowote wa kutupa mikopo?
Read More
Answer: Asante saana kwa pongezi. NICOL kama taasisi haihusiki na biashara ya kutoa mikopo kwa wanahisa wake au wananchi. Lakini hisa za NICOL zinaweza kutumika kama dhamana katika taasisi mbali mbali kifedha kama benki.
REGINA MACHUA: Ningependa kujua je, gawio linatolewa kila mwaka?
Read More
Answer: Gawio linatolewa pale kampuni inapopata faida. Bodi ya wakurugenzi itapendekeza gawio ambalo litaidhinishwa katika mkutano mkuu wa wanahisa.
GREGORY GERALD NZUGURUQuestion:Kiuhalisia tunaomba kutumiwa vitabu vya Nicol ,lakini pia certificate mpya.
Read More
Answer : Tunafanya utaratibu wa kuweka vitabu vyote kwenye tovuti yetu ili wanahisa wote wavipate kwa urahisi. Vyeti vya wanahisa vinapatikana kupitia kwa mawakala/madalali wa soko la hisa (Stock market broker)
GREGORY GERALD NZUGURUQuestion2:Tunaomba pia kujua Hisa kwa Sasa zipo kiasi gani, kila mtu atumiwe kiasi Cha Hisa zake.
Read More
Answer:Thamani ya hisa kwa sasa ni 250 kwa hisa.
GREGORY GERALD NZUGURUQuestion 3:Tunaomba kupewa vitambulisho ambacho kitakufanya ujulikane Kama mwana Hisa.
Read More
Answer: CHeti cha hisa ni kitambulisho cha mwanahisa.Tunaamini unacho cheti cha hisa kinachokutambulisha kuwa mmiliki wa hisa za NICOL.
EXPELIUS BANZI KUNIQuestion: Tafadhali sahihisha jina kwa mawasiliano ya baadaye Jina langu sahihi ni :- Expelius Banzi Kunambi
Read More
Answer:Tumepokea masahihisho hayo.Tunashauri uwasiliane na mawakala wasoko la hisa ili waweze kukupatia muongozo wa kusahihisha cheti cha hisa kiwe kwenye jina sahihi.
WILFRED WILLIAM MATONYAQuestion: Bravo NICOL management! But consider those who cannot access this broad cast meeting. All the Best!!!
Read More
Answer:Thank you and well noted.
JULIUS LUTA MUSHUMBAQuestion: Kwa njia hii ya Mtandao ilitakiwa kutumiwa agenda na muhutasari wa mkutano uliopita, ili iwe rahisi kuchangia au kujua mwelekeo wa mkutano. Kwa hali hii ni njia ya kwendelea na meeting bila faida ya mjadala wenyewe. Mwisho kuna wanachama hawana na au hawajui kutumia hìi njia hivyo WAMENYIMWA HAKI YA KUCHANGIA.
Read More
Answer: Tumepokea maoni na tunashuhulikia.
: SAMSON MENYASUMBA MOLELAQuestion: Habari swali langu, ni nini kinachoendelea kwa sasa?
Read More
Answer:Tunaendelea kutoa magawio ya mwaka 2016,2017,2018 na 2020 pia shuhuli za uwekezaji zinaendelea.
JULIUS LUTA MUSHUMBAQuestion: Kwa sisi ambao hatuna masanduku ya posta ya kupitishia BARUA NA VIFURUSHI, itakuwaje ikifika muda wa kupata HARDCOPY?.
Read More
Answer: Taarifa zote zitakuwa zinawekwa kwenye tovuti yetu ili kurahisisha upatikanaji wa document za kikao. Pia Hard copy zinapatikana ofisini, wanahisa waliopo maeneo ya jirani waweze kuzichukua.
JUMANNE AMAN JUMA NSATOQuestion: Toka mwaka 2006 nilpojiunga na shilika sikapata gawio lolote wala taarifa yoyote kuhusu shirika pia nilileta taarifa zangu baada ya kusikia tangazo la kugawia mgao wa miaka 3 kuanzia 2016 mpaka 2018 akaunti namba nilitoa
Read More
Answer: Tumeanza kulipa gawio la mwaka 2016,2017,2018 na 2020 nayote ulilipwa kupitia akaunti yako TPB tarehe 1/6/2021.
DOMINIC MUNGA MATHIASQuestion: Congratulations NICOL for this attainment. My question: Last year 2019, I remember to have filled a prescribed form and submit to you showing my bank account particulars for you to deposit my share dividends according to your instructions.Since then I haven't got any information if you really made the deposits or not and how much was that if any. Thanks and best regards.
Read More
Answer:Thank you.Your dividends has been paid through your equity bank account as follow year 2016 amont paid 4750 29/5/2019,year 2017 amaunt paid 4,940 27/5/2019,year 2018 amount paid 1,140 28/12/2019 and 2020 amont paid1900 14/2/2020
JONES MANDAGO SHINDIKAQuestion: Naomba kujua namna ya kuuza hisa zangu.
Read More
Answer: Ili uweze kuuza hisa zako, fika katika ofisi za madalali wa soko la hisa ukiwa na cheti cha hisa pamoja na nakala ya kitambulisho chako.
DAISY HARRIET LWETAKAQuestion: Habari! Naitwa Daisy Lwetaka. Napenda kufahamu mnatumia utaratibu gani kuwafikia au kuwasiliana na wanahisa ambao hawana uwezo wa kutumia mawasiliano haya. Pili tangu ninunue hisa na kupata certificate sijawai kupata taarifa ya nini kinaendelea wala gawio mpaka nilivyoona kwenye mitandao na kutuma details zangu.
Read More
Answer: Tunatumia njia ya simu,barua na barua pepe kuwafikia wanahisa.wasiliana na mawakala wasoko la hisa kupata muongozo juu ya utaratibu wa kupata cheti.
VIVIAN TEOGNUS MAKUHANAQuestion: Hongera sana NICOL kwa hatua hii.Member aloyeuliza kuhusu ripoti zilizopita zipo katika pdf.
Read More
Answer: Ahsante sana.Tembelea tovuti yetu www.nicol.co.tz ili kupata ripoti zote zilizowahi kutolewa
ROBERT RAPHAEL RWEZAURAQuestion: Hivi kwa Mwaka 2018,2019 Gawio halikutoka? Maana sijapata mimi.
Read More
Answer:Gawio limetoka mwaka 2016,2017,2018 na 2020.Gawio la mwaka 2018 umelipwa kupitia akaunti yako ya NMB shilingi 49’400.2019 hakukuwa na gawio.
REGINA MACHUAQuestion: Nikitaka kuchukua hela kidogo nafanyaje?
Read More
Answer:Hela unapata kwa njia mbili1.tunapolipa gawio 2.unapouza hisa zako.
JAMES MNEESI TERIQuestion: Administrative expenses - are they not on the high side eating on profits and dividends? Board needs to look into this I think
Read More
Answer:Thank you for your question, the Board took note
NESTORY MATHEW NYAMUGOLEQuestion: Mimi Kama mwanahisa naweza kupata mkopo.
Read More
Answer:NICOL kama kampuni haina taratibu ya kukopesha ila unaweza kutumia hisa zako kama dhamana ya mkopo wako katika taasisi utakayochagua kukopa.
MWADHINI SALM KIMOMWEQuestion: Mbona taarifa za mkutano hazijtoka mapema ili tujue namna ya kujaza fomu za uwasilishaji, na La pili tunaomba tujue utaratibu wa mgao wa hisa,Tati naomba kujua Kua Sisi katika NICOL tuna kitega uchumi gani, Naomba kujua kiasi cha shea ili kujua ni namna gani tutaweza kuuza au kununua shea.
Read More
Answer:Matangazo ya mkutano hutangazwa kupitia magazeti,redio na televisheni siku 21 kabla ya mkutano.Utaratibu wa mgao wahisa ni unatakiwa kuhakiki taarifa zako kwa kujaza fomu ya uhakiki zinazopatikana ofisini kwetu au kupitia tovuti yetu.Kujua kuhusu vitegauchumi vyetu,pitia tovuti yetu www.nicol.co.tz kupata ufafanuzi zaidi.
RAPHAEL ERO MUHEQuestion: RAPHAEL MUHE HISA NUMBER 14990: KWANINI VIKAO NI DAR ES SALAAM TU
Read More
Answer:Kutoka na changamoto ya UVIKO 19 mikutano tumeanza kufanya kwa njia ya mtandao.Hali ya unjonjwa huu itakapo kaa sawa tutatengeneza utaratibu wa kufanya nje ya Dar es Salaam.
SAMUEL DHAHABUQuestion: Inachukua muda gani hadi kupata gawio lingine?
Read More
Answer: Gawio linatolewa pale kampuni inapopata faida. Kampuni ya NICOL imeweka utaratibu wa kutoa gawio katika robo ya mwisho wa mwaka.
ANDREW GAMALIEL TESHAQuestions: 1. Since 2016 there has been a steady decline in Income and Net Profit, leading to earnings of only TZS1 per share in 2019. What short to medium term strategies does the Management have to stop this decline in revenue, and reverse the trend?
Read More
Answer:1 The Board and Management took various steps to improve earnings of the company including dropping all non profit business segment which for some reasons was the reasons for declining performance in previous years.
ANDREW GAMALIEL TESHAQuestions: 2 In the long-term there is a plan to diversify the investment portfolio heading towards 2025 which includes marked increase in investments in Fixed Deposits, Government Bonds and Treasury Bills. How is the Board and Management planning on capitalizing this investment strategy?
Read More
Answer: 2As approved by the shareholder, the diversification plan will be made by diversifying to start with disposing some 6 million shares of NMB and the proceeds to be invested in the Government Bond. This diversification program will be reviewed on an annual bases and reported to the shareholders in the Annual General Meeting.
ANDREW GAMALIEL TESHAQuestions: 3 The investment strategy from a risk perspective is commendable to guarantee returns of between 8-16% annually for shareholders, however as a growth strategy for the company may not markedly increase the capital base once operational and other costs are taken into consideration. What other growth strategies has the management considered to significantly increase earnings and the company's capital base?
Read More
Answer: 3 Management considers diversification program once achieved is expected to widen sources of earnings and guarantee consistent company’s earning and thereafter enhancing an increase of capital base through re-investment of earnings.
GREGORY GERALD NZUGURUQuestion: Tunaomba Wana Hisa tupewe mikopo
Read More
Answer: Kampuni haitoi mikopo kwa wanahisa wake ila hisa zako zinaweza kutumika kama dhamana katika taasisi zinazotoa mikopo kama watakubaliana na dhamana hiyo.
RWEGASIRA PETER ZIMBEIYAQuestion: Hii habari ya TMCL mnaweza kutukumbusha vizuri mchakato wake.... tumepoteza vipi umiliki wakati kuna pesa tumeiweka hapo zaidi ya 1B
Read More
Answer:Ni kweli Mr Zimbeiya, NICOL ilipoteza udhibiti wa kampuni ya TMCL mara tu Waziri wa Mifugo alipotoa amri ya kunyang’a nya mali za TMCL na kuziweka chini ya Wizara ya Mifugo, hata hivyo uongozi wa NICOL umepinga hatua hii na hatua za kisheria zinaendelea kudai haki ya NICOL.
YUSUPH MOHAMED SADICKQuestion: Had seen we have declare payment of dividends 10 per share but had reviewed the account for 2019 have no profit we these dividends come from.
Read More
Answer: TZS 10 per share declared is for interim dividend for the year 2020.
RWEGASIRA PETER ZIMBEIYAQuestion: Hisa mbona zinashuka trend yake si nzuri uongozi mnalakufanya hapo...
Read More
Answer:Kushuka na kupanda kwa bei yah isa sokoni inategemea na uhitaji wa hisa kwa wanunuzi na wahitaji sokoni.
ANTONY AMBIKILE NSOJOQuestion: Naomba tufafanuliwe kuhusu TMCL -what was the issue? na ilikuwaje tukapoteza.
Read More
Answer: NICOL ilipoteza udhibiti wa kampuni ya TMCL mara tu Waziri wa Mifugo alipotoa amri ya kunyang’a nya mali za TMCL na kuziweka chini ya Wizara ya Mifugo, hata hivyo uongozi wa NICOL umepinga hatua hii na hatua za kisheria zinaendelea kudai haki ya NICOL.
MAGDALENA JUBLATE MUNISIQuestion: Magdalena jublate tunaomba kujua maendeleo ya Nicol hatujui kwa miaka mingi sasa
Read More
Answer:Kwa sasa Nicol inaendea kuwekeza sehemu mbalimbali,ila pia tumekuwa tukifanya mikutano mikuu kila mwaka ili kuweza kujadiliana na wanahisa mambo mbalimbali yanayohusu kampuni na tunaendelea kutoa magawio yam waka 2016,2017,2018 na 2020.
CHARLES DANIEL MKUMBOQuestion: Naomba kuuliza "katika shughuli za uwekezaji maana yake kunawekezwa sehemu nyingi zenye forecast Ed potentially profit sio kuwekeza kwenye huduma ndio maana tumepata hasara kirahisi kampuni moja tu iliyotetereka isingesha faidi hivyo tuelezeni sababu ya kina!
Read More
Answer:Tunashukuru kwa swali lako zuri, hata hivyo kampuni ya NICOL kwa sasa inajikita haswa katika uwekezaji wenye tija ambao utaongeza thamani kwa kuzingatia sera za uwekezaji.
DANIEL OLE NJOLAIQuestion: Kuna haja ya kujenga hoja ili serikali itu refund hisa zetu 51% za tmcl, na mkopo tulioutoa kwa kampuni
Read More
Answer:Ushauri wako ni mzuri sana, kampuni imechukua hatua kadhaa kuhakikisha kuwa maslahi ya NICOL katika umiliki wa 51% TMCL unalindwa. Hivi sasa suala hili lipo mahakamani.
GASPER BAITWAQuestion: KUHUSU KIFUNGU 6.7 KWA WANAHISA KUPITISHA MAPENDEKEZO YA KUPITISHA MALIPO YA WAKURUGENZI NA VIFURUSHI VYAO; MIMI KWA MAONI YANGU NIKIWA MWANA HISA VIWANGO HASA VIFURUSHI KUHUSU VIKAO, SAFARI NAKADHALIKA VINGEBAKIA VILE VILE KAMA ILIVYO MWAKA 2019, KULIKO KUONGEZA, ILI KUSUDI SISI NASI WANAHISA TUFUTIWE JASHO NA KUWA TUMEKUWA WAVUMILIVU KWA KUPATA GAWIWO LA SHS.10/= KWA KILA HISA KAMA ILIVYO KUWA MWAKA JANA. NINGEPENDEKEZA ANGALAU SHS.30/= KILA HISA. Gasper Peter Baitwa (163340)
Read More
Answer: Asante tumepokea maoni yako, tutafikia huko.
REGINA MACHUAQuestion: Je nicol ilijitoa NMB bank?
Read More
Answer: Hapana, NICOL bado ni mwanahisa wa benki ya NMB.
GASPER BAITWAQuestion: PIA NINA WAPONGEZA KUPATA FAIDA BAADA YA KODI KWA KIPINDI HIKI KILICHO ISHIA 30.06.2020 KWA PATO LAFAIDA YA SHS. 2,903,167,000/= BALI YAMKINI WA GAWIWO LA KWA MWANAHISA LIGEFIKILIWA KUPANDISHWA KAMA NILIVYO WAKUTOA MAONI HAPO AWALI. Gasper Peter Baitwa. (163340).
Read More
Answer:Tumepokea maoni yako na tunashuhulikia.
: KYUZA JOSEPH KITUNDU
Read More
Hongereni sana ni biashara nzuri isiyo na hasara-Kyuza Joseph Kitundu
ANDREW GAMALIEL TESHAQuestion: Kuhusu swala la kuondoloewa wanahisa, je mwanahisa akijitokeza kutokana na taarifa za mkutano huu, ni kwamba bado hisa zake zitafutwa pamoja na kwamba alitoa fedha taslimu kisheria kumiliki hizo hisa na kupewa uthibitisho?? Wengine wameshafariki, wengine hawapo tena nchini, makazi na namba za simu zilibadilika. Wengine warithi wao pengine wana haki ya kumiliki hizo hisa lakini hawajawahi kupata hizi taarifa. Sio kila mtu anasoma kila gazeti kila siku, ni rahisi kutopata hizi taarifa kuliko kuzipata kama mawasiliano hazikufanyika moja kwa moja na mwanahisa. Bodi kwenye hili inasemaje, zisije zikatokea mashtaka na malalamiko baadaye na wanahisa halisi juu ya hili. Pendekezo ingewekwa "caveat" kwa mwanahisi atakaye weza kuthibitisha ununuzo wa hisa zake usio na kikomo, kama vile iliyopo kwa gawio ambazo hazijapokelewa na wanahisa, kwa wengine ata tangu kampuni ianze. Asante.
Read More
Answer: Kabla ya kutoa pendekezo la kuzifuta tulifata utaratibu wa kuwaandikia barua wanahisa wote wenye hisa zinazotakiwa uthibitisho wa manunuzi ya hisa hizo.Wapo walio hakiki na wapo ambao hawakujitokeza, hata hivyo tumepokea maoni yako.
DANIEL OLE NJOLAI
Read More
Baada ya maelezo ya Mwenyekiti, nakubaliana kwamba tuzingatie ushauri wa kitaalam la LIQUIDATION.
: JAMES PHILBERT MPELETunawashukuru sana Viongozi wetu. Mimi naomba mdumishe utamaduni wa kuwasiliana na wana-hisa kwa kila jambo linalofanyika juu ya hisa zetu.
Read More
Answer:Ahsante kwa ushauri,tumeupokea na tutaendelea kuufanyia kazi.
JAMES PHILBERT MPELEQuestion: Official website ya NICOL ni ipi? Tuelezeni wana-hisa physical location ya ofisi zenu/zetu. Hizi documents mnaweza kuzipost kwenye website ya NICOL, au kama zitakuwa siyo kwa ajili ya public tutumieni kwenye e- mail zetu.E-mail yangu ni: mweyujames@gmail.com.
Read More
Answer: Tovuti ya NICOL ni www.nicolplc.co.tz, Makazi ya ofisi ni katika ghorofa ya tatu, Jengo la “Mirambo House” Mtaa wa Mirambo. Documents zote za mkutano zitawekwa kwenye tovuti ya kampuni.
KAUWED GAMALIEL SHAOQuestion: Naomba maelezo kuhusu kiwanda cha nyama cha Dodoma ambacho nasikia kilichukuliwa na serikali, ni kwa nini na nicol imepata mgao gani?
Read More
Answer: NICOL ilipoteza udhibiti wa kampuni ya TMCL mara tu Waziri wa Mifugo alipotoa amri ya kunyang’a nya mali za TMCL na kuziweka chini ya Wizara ya Mifugo, hata hivyo uongozi wa NICOL umepinga hatua hii na hatua za kisheria zinaendelea kudai haki ya NICOL.
SAMUEL DHAHABUQuestion: Ni nani anayeshuhulika na hisa mwanza,
Read More
Answer:Ofisi ipo Dar es Salaam ila tunatoa huduma kwa mikoa yote kwa njia ya barua pepe,simu,barua na kwa njia ya mtandao.
MESHACK MTIVIKE MWENDAQuestion: kwanini msiite watu wakahudhulia mkutano badala ya kuitisha kwa electronic.
Read More
Answer: Kutokana na janga la uviko19 na maagizo ya serekali ya kutokuwa na mikuanyiko.
PAUL NYITIKA CHAMAQuestion: je unaposema unafuta hisa ambazo wanahisa wake hawajaonesha risiti zao za malipo unafuta kwa vigezo vipi????
Read More
Answer: NICOL ilitoa muda wa kuwasilisha nyaraka za kudhibitisha umiliki halali wa hisa hizo, na kwa kuzingatia historia ya NICOL upo uwezekano kutokea kwa makosa wakati wa utoaji wa hisa mwaka 2005, hivyo ni muhimu kufanya marekebisho.
EVELYNE MBARAKA IKELEKO(ADMIN) ANTHONY GERSON MELELE(DECEASED)Kikao mtandaoni ni kizuri sana Naomba tupewe taarifa mapema zaidi ili mtu ajipange kufuata network ilipo EVELYNE MBARAKA KELEKO (ADMIN) ANTONY GERSON MELELE (DECEASED) CDS A/C NO 175150
Read More
Answer: Asante kwa ushauri wako. Tutalizingatia hili katika mkutano mkuu ujao.
YUSUPH BAKARI MHANDOQuestion:1. Kwanini TMCL imesamehewa deni bila ya maelezo ya kutosha, na TMCL imesamehewa deni kwa interest ya nani?
Read More
Answer: TMCL haijasehewa deni bali NICOL imejitoa kuwa mwanahisa/mmiliki wa TMCL. Bado tunaendelea na taratibu za kisheria kujitoa katika umiliki wa TMCL.
OMARY YUSUF NGAYENDANashauri tusiwekeze kwenye miradi inayoendeshwa na serikali political risk ni kubwa Sana hasa nchi zetu
Read More
Answer: Asante sana kwa ushauri wako. Tutalizingatia hilo katika uwekezaji kwenye miradi hapo baadae.
ANTONY AMBIKILE NSOJOQuestion: Hivi uamuzi wa kuinvest kwenye campuni fulani huwa unaangalia vigezo gani? Nahisi kuna shida kwenye uchaguzi wa wapi pa kuwekeza.
Read More
Answer: Uamuzi wa kuwekeza katika kampuni fulani unategemea na aina ya kampuni, mtaji unaohitajika katika kampuni husika.
: RWEGASIRA PETER ZIMBEIYAQuestion: Validation za hisa zinafanyikaje na mwisho ni lini?
Read More
Answer: Uhakiki wa hisa bado unaendelea.
EVELYNE MBARAKA IKELEKO(ADMIN) ANTHONY GERSON MELELE(DECEASED)Question: Na siyo watu wote wenye uelewa wa mambo ya hisa kwani wengine ni warithi wa hisa na watoto wako vijijini na hawana msaada wa kufika ili kupata haki wanafanyaje? EVELYNE MBARAKA IKELEKO(ADMIN) ANTONY GERSON MELELE (DECEASED) CDS A/C NO.170174 Naomba kusaidiwa
Read More
Answer: Tumekuwa tukitoa matangazo ya kuelekeza ofisi zilipo ila tumekuwa tukitoa namba za simu,anwani na anwani ya barua pepe mara kwa mara kupitia magazeti,redio na luninga ili kuweza kuwafikia wanahisa wet una kutatua matatizo yao yanayohusu hisa.
SAMWEL HAPPYSON SWAINaomba kushauri pia tungee angalia sekta ya makazi ( Real estate sector) au sekta ya gesi ya majumbani( Cooking Gas sector) pia Sekta ya nishati kama umeme (Electricity Energy Sector) Maana ni maeneo yanayokuwa kwa kasi sana katika uchumi wa viwanda kwa sasa
Read More
Answer: Asante kwa ushauri wako. Tutazingatia hili tutakapokuwa tunaongeza wigo wa uwekezaji wetu.
TIM SANDEMAN STAERMOSERecommendations
Read More
For those chasing dividends or information on shareholdings, per the annual report, you can contact: The Registrar, CSD & Registry Company Limited, 2nd Floor, NHC Corporate Office, Kambarage House, 6 Ufokoni Street, P.O. Box 70081, Dar es Salaam, Mobile 0746 160 516, Email registrar@csdr.co.tz. It has been two years and 4 months or so since NICO relisted at the DSE. This is the third AGM since relisting. One would hope ample opportunity has been afforded to people to come forward and prove share ownership, and if so, collect the dividends they are rightfully entitled to -- which can only be paid directly into a bank account or mobile money account in the name of the registered shareholder. If anyone wants to contact me, I am happy to discuss NICO any time: Tim Staermose, staermo@gmail.com It's our company. We need to make sure it performs to the best of its potential and we all share in the results of that.
SOPHIA SWEDI GURTUQuestion: mimi naomba kufahamu magiwio ambao yameshatolewa tangu kuanzishwa kwa NICOL
Read More
Answer: Gawio ambalo limeshatolewa ni kama ifuatavyo; Mwaka 2016 – Sh. 25, Mwaka 2017 – Sh. 26, Mwaka 2018 – Sh. 6, Mwaka 2020 – Sh. 10
FAUSTINE WILLYBROAD KILONGOQuestion: Nashukuru tumepata gawio. lakini sielewi ni vigezo gani linatolewa. mmesema ni shilingi kumi kwa hisa au kwa vigezo gani?
Read More
Answer: Gawio linatokana na faida ya mwaka husika,vigezo vya kupata gawio ni uwe mwanahisa halali wa kampuni ya NICOL.
CHARLES DANIEL MKUMBOQuestion: Wengi bado tunavyo vyeti vya zamani na kwa sasa idadi ya hisa zimebadilika naomba kujua nitapataje cheti kipya chenye kuendana na idadi za hisa sasa zilivyo
Read More
Answer:Vyeti vyote vilitolewa na kutumwa kupitia masanduku ya posta ya wanahisa.Kama hauna cheti unatakiwa kuwasiliana na mawakala wa soko lahisa kwa utaratibu wakupatiwa cheti.
: SOPHIA SWEDI GURTUQuestion: naomba kupata ufahamu kuhusu hisa za DSE na hisa NICOL maana mm na hisa kote naomba maelekezo
Read More
Answer: NICOL ni kampuni ambayo imeorodheshwa katika soko la hisa Dar es Salaam (DSE). Pia Dar es Salaam Stock exchange (DSE) ni kampuni ambayo imeorodheshwa katika soko la hisa Dar es Salaam. Hivyo basi, inawezekana kuiliki hisa za kampuni zote mbili kwa sababu zimeorodheshwa katika soko la hisa Dar es Salaam
DANIEL OLE NJOLAI
Read More
Nayaridhia maazimio yote ya AGM
DISMAS NANNA RUGUDAGIZAQuestion: wakati nilipotembelea ofisini kwenu niliambiwa kwa waanzilishi kwa kuwa imepita mda mrefu kufidia huo mda share zitakuwa doubled na certificate hazikutolewa za hizo additional share nahitaji maelezo juu ya hili
Read More
Answer:Cheti chako kipo ofisini kwetu.Tafadhali wasiliana nasi ili kukupa utaratibu wa kupata cheti hicho.
DISMAS NANNA RUGUDAGIZAQuestion: kwa miaka ya nyuma share kama zilikuwa zinatolewa sisi ambao hatukuzipata tunafanyaje?
Read More
Answer:Tumetoa gawio kuanzia mwaka 2016.Utaratibu wa kupata gawio ni kama ifuatavyo.Unatakiwa kujaza fomu ya uhakiki ambayo inapatikana ofisini kwetu au kupitia tovuti yetu www.nicol.co.tz
ANTONY AMBIKILE NSOJOQuestion: Havent heard of any further strategic investments. Au tumetosheka na hapa tulipo?
Read More
Answer: Currently NICOL has been investing in government boinds. In addition to that, There are other Investments in various sectors which are still in the pipeline. Shareholders will be notified when the company ventures into these investments.
SAMUEL NYAMBEHO MTOKAmkutano ulikuwa mzuri honereni wote kwa kushiriki
Read More
Answer:Ahsante sana.
Previous
Next